PSG yaja ya MCN kibo ya MSN ya Barca

Muktasari:

  • PSG na Man City ndizo klabu zilizofunga mabao mengi zaidi katika ligi kubwa tano barani Ulaya

Sahau kabisa MSN ya Barcelona habari mjinia sasa ni safu ya ushambuliaji wa Paris Saint-Germain inayoundwa na Neymar, Edinson Cavani na Kylian Mbappe (MCN) imeshiriki kufunga na kutegeneza  mabao 29 yaliyofungwa na timu hayo.

Katika misimu minne iliyopita safu ya ushambuliaji iliyokuwa ikiogopewa zaidi ni MSN ya Barcelona iliyokuwa ikiundwa na Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar kwa misimu hiyo iliweza kuweka rekodi ya kufunga mabao zaidi ya 100 kwa msimu.

Baada ya kuondoka Neymar katika klabu ya Barcelona msimu huu kwa uhamisho uliovunja rekodi amehamishia makali yake ya miamba ya Ufaransa.

Katika Ligi ya Mabingwa, PSG imeweka rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi 12 katika mechi tatu  na MCN wakifunga mabao tisa hali inayofanya nyota hao kuonekana kama wamekuwa pamoja kwa muda mrefu kumbe ndiyo kwanza wanamiezi pamoja.

Washambuliaji hao wamecheza mechi sita pamoja na wamefanikiwa kufunga mabao 17 katika michezo hiyo.

"Cavani ni mchezaji nora na Kylian ni nyota," alisema Neymar.

"Bado tuna mengi ya kujifunza na kubadiliki tunatakiwa kufanya kazi zaidi kwa sasa."

Pamoja na kauli ya Mbrazil huyo, lakini namba zinasema tofauti pamoja na kuwepo kwa sintofahamu kati yake na Cavani.

Safu ya MCN wanatagemewa kuifungia PSG mabao zaidi ya 43 katika msimu huu baada ya kuhusika katika asilimia58% za magoli yote hadi sasa.

"Nafurahisha na uchezaji wa mchezaji moja moja, lakini tunatakiwa kufanya kazi kwa umoja," alisema kocha Unai Emery.

Jijini Anderlecht, Mbappe alikuwa mchezaji chipukizi zaidi kufunga mabao mengi katika historia ya Ligi ya Mabingwa na Cavani akifunga katika mechi saba mfululizo wakati Neymar akikaribia kuweka rekodi mpya katika mashindano hayo.

Rekodi ya mabao ya MCN katika mechi sita zilizopita

  1. Metz 1-5 PSG: Mbappe (bao moja), Cavani (mawili) na Neymar (moja)
  2. Celtic 0-5 PSG: Mbappe (moja), Cavani (mawili) na Neymar (moja)
  3. PSG 2-0 Lyon: Watatu hao hawakufunga bao lolote
  4. PSG 3-0 Bayern: Mbappe (hakufunga), Cavani (moja) na Neymar (moja)
  5. PSG 6-2 Bordeaux: Mbappe (bao moja), Cavani (moja) na Neymar (mawili)
  6. Anderlecht 0-4 PSG: Mbappe (bao moja), Cavani (moja) na Neymar (moja)