Lwandamina anaangalia pointi tatu tu

Muktasari:

Yanga ilipata ushindi wa mabao 5-0 mwishoni mwa wiki iliyopita, ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi na pointi 20 nyuma ya Simba inayoongoza na pointi 22 ambazo ni sawa na Azam FC inayoshika nafasi ya pili.

Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina amesema, anachoangalia ushindi na pointi tatu tu, na kuhusu mabao mengi ni kwa ajili ya kuwaongezea wachezaji wake hali ya kujiamini.

Lwandamina ambaye ni Mzambia amesema, anachoangalia ndani ya kikosi chake ni ushindi wa pointi tatu na siyo idadi ya mabao kwa sababu ushindi wa namna hiyo ni kwa ajili ya kuongeza hali ya kujiamini.

"Katika mchezo unachokiangalia ni pointi tatu tu, ukishinda bao moja na matano pointi ni zile zile, lakini uzuri wa kuwa na idadi kubwa inasaidia kuwajenga wachezaji kuwa na hali ya kujiamini,"alisema Lwandamina.

"Hata hivyo ni kawaida kwa kocha kufurahia timu inapofanya vizuri, tunashukuru na lengo ni kuona tunafanya vizuri kila mchezo na kusonga mbele zaidi."