Lulu atoa zawadi kwa watoto ‘Birthday’ yake.

Monday April 16 2018

 

By Rhobi Chacha

Dar es Salaam. Siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Msanii wa Bongo Movie, Elizabeth Michael 'Lulu' anayetumikia kifungo gerezani imefanyika leo Jumatatu kwa kutoa zawadi kwa watoto walio na vichwa vikubwa waliolazwa katika Hospital ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Zawadi hizo zimewakilishwa na mama yake Lulu pamoja na msanii mkongwe wa filamu, Dr Cheni.

 Mbali ya kutoa zawadi hizo pia Lulu alitoa ujumbe wa kuwafajiriji wagonjwa hao pamoja na wazazi wao.

Ujumbe huo wa Lulu ulisomwa na Dokta Cheni umesema "Anawapenda sana, nawaombea na naamini mkiwa huru na kumuomba Mungu basi haya maradhi yatakuwa ya muda mfupi  na afya za watoto zitakuwa nzuri, nawatakia kila la kheri na mpone haraka."

Kwa mujibu wa Dokta Cheni alisema Lulu siyo mara yake ya kwanza kuja kutoa zawadi kwa watoto hawa wenye vichwa vikubwa kwani, imekuwa akifanya hivi kila wakati ifikapo siku yake ya kuzaliwa.