Lulu Michael hataki tabu na mtu

Muktasari:

  • Watu mitandaoni walianza kupiga domo hasa kutokana na kupungua kwa kupostiana katika mitandao ya jamii kama mwanzo ilivyokuwa.

WAKATI watu wakiendelea kupiga domo juu ya uhusiano wa Lulu na Majizzo kwamba yameota mbaya mwenyewe ametulia hataki makuu.

Watu mitandaoni walianza kupiga domo hasa kutokana na kupungua kwa kupostiana katika mitandao ya jamii kama mwanzo ilivyokuwa.

Majizzo aliamua kukata hali hiyo baada ya kuposti picha katika mtandao wake wa Instagram akiwa pamoja na Lulu, huku akiandika "Umekwiza CEO".

Naye Lulu katika komenti akajibu "Nikushukuru kwa mafunzo Mwalimu Ubarikiwe Mwaya" na hiyo kuonesha wawili hawa bado mambo yapo moto moto kwa upande wao.