Lulu Diva na Rich Mavoko waanika kila kitu

Muktasari:

Wawili hao walihudhuria hafla ya uzinduzi wa kipindi hicho cha 'Nyumba ya Imani' ambacho kitarushwa moja kwa moja na Wasafi TV inayomilikiwa na mwanamuziki Bongo Fleva,  Naseeb Abdul 'Diamond Plutnumz'.

Dar es Salaam: Baada ya kusambaa kwa tetesi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, mwanamuziki, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, anatoka kimapenzi na mwanamuziki mwenzake, Richard Martin ‘Rich Mavoko’, jana Jumapili katika uzinduzi wa kipindi cha 'Nyumba ya Imani' wawili hao walikuwa kivutio mbele ya waalikwa waliofika kuhudhiria hafla hiyo.

Wawili hao walihudhuria hafla ya uzinduzi wa kipindi hicho cha 'Nyumba ya Imani' ambacho kitarushwa moja kwa moja na Wasafi TV inayomilikiwa na mwanamuziki Bongo Fleva,  Naseeb Abdul 'Diamond Plutnumz'.

Pamoja na kudai ni tetesi na si wapenzi, wawili hao waliingia pamoja katika uzinduzi huo na kwenda kukaa sehemu moja huku muda mwingi walikuwa wakionekana wakionyeshana kitu kwenye simu zao na wakati mwingine wakijipiga picha na kufanya  baadhi ya watu waliokuwapo hapo wakiwatazama.

MCL Digital ilipata nafasi ya kuongea na Lulu Diva amesema: “Mimi na Rich hatujawahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi, ni mtu wangu, tunasaidiana kwenye kazi na ndiye aliyenitungia wimbo wangu mpya wa Ona."

"Kuhusu mapenzi hakuna ukweli, sema watu wanapenda iwe hivyo, ila wajue kila mtu ana mpenzi wake,” alisema Lulu Diva anayetamba na wimbo huo wa Ona.