Lukaku apiga mbili, Ubelgiji yaua

Muktasari:

Hii ni mara ya kwanza kwa Ubelgiji na Panama kukutana katika Kombe la Dunia

Moscow, Russia. Mshambuliaji Romelu Lukaku amefunga mabao mawili na kuiongoza Ubelgiji kuichapa Panama 3-0 katika mchezo wa kwanza wa Kundi G.

Ubelgiji ikiwa na nyota wake wote walibidi kusubiri hadi kipindi cha pili kufanya kile kilichotegemewa na wengi katika mchezo huo.

Kiungo Mertens alifungia Ubelgiji bao la kwanza kwa shuti la mbali kabla ya Lukaku kupachika mabao yake akitumia vizuri krosi ya Kevin de Bruyne na Eden Hazard.

Ubelgiji ilinufaika na mbinu yao ya kushambulia kwa kushtukiza wakitumia kasi ya Bruyne na Hazard waliokuwa mwiba kwa ngome ya Panama.

Katika mchezo kipa wa Panama, Penedo alifanya kazi kubwa katika kipindi cha kwanza kuzuia mashambulizi ya Ubelgiji.

Kiungo wa Chelsea, Hazard ameweka rekodi ya Kombe la Dunia kwa kucheza pamoja na ndugu yake Thorgan Hazard aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mertens.

Matokeo hayo yanaifanya Ubelgiji kuongoza kundi hilo kabla ya mchezo kati ya England na Tunisia.

Vikosi

Ubelgiji: Courtois, Alderweireld, Boyata, Vertonghen, Meunier, De Bruyne, Witsel, Carrasco, Mertens, Eden Hazard, Lukaku.

Akiba: Mignolet, Vermaelen, Kompany, Fellaini, Thorgan Hazard, Tielemans, Januzaj, Dembele, Batshuayi, Chadli, Dendoncker, Casteels.

Panama: Penedo, Murillo, Roman Torres, Escobar, Davis, Barcenas, Cooper, Gomez, Godoy, Jose Luis Rodriguez, Perez.

Akiba: Calderon, Cummings, Gabriel Torres, Diaz, Machado, Pimentel, Arroyo, Ovalle, Tejada, Avila, Baloy, Alex Rodriguez.

Mwamuzi: Janny Sikazwe (Zambia)