Lipuli FC yapambana na Kamati ya Saa 72

Wednesday September 13 2017

 

By Justa Musa

Mbeya.  Uongozi wa Klabu ya Lipuli FC ya Iringa umepinga uamuzi uliyotolewa na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi Kuu maarufu Kamati ya Masaa 72 baada ya kutupilia mbali ombi la kufutwa kwa kadi nyekundu aliyopewa mchezaji wao, Asante Kwasi.
Asante alipewa kadi hiyo na mwamuzi baada ya kulalamika kupigwa na kiungo wa Yanga Raphael Daudi, mechi ambayo timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Klabu hiyo ya Iringa, Clement Sanga imedai baada ya mchezo, uongozi wa Lipuli uliandika barua ya kuipinga kadi hiyo ambayo Kwasi alionewa.