Linah aapa kuanika picha akipata ujauzito mwingine

Muktasari:

  • Akifunguka katika mahojiano na na mwandishi alisema kwamba yeye anafanya anachojisikia na kukiri endapo akipata ujauzito mwingine atapiga picha zingine sababu yeye ni maarufu na anajisikia kufanya hivyo.

MWANAMUZIKI ambaye kwa sasa ni mama wa mtoto mmoja, amewapiga dongo waliokuwa wakimfuatafuata kipindi alipokuwa na ujauzito hasa kutokana na picha alizopiga kwa kipindi hicho.

Akifunguka katika mahojiano na na mwandishi alisema kwamba yeye anafanya anachojisikia na kukiri endapo akipata ujauzito mwingine atapiga picha zingine sababu yeye ni maarufu na anajisikia kufanya hivyo.

Aidha pia aliongeza kuwa hababishwi na watu wanavyoongea sababu hakuna mtu anaempangia maisha yake sababu yeye yupo kupamba na hali yake tangu muda sana kwa hiyo nao wapambane na hali zao.

“"Binadamu ni watu wa ajabu sana na hata ufanye nini huwezi kuwaridhisha kwa kuwa kila mtu anatamani ufanye kile anachokitaka yeye nikivaa gauni refu watasema mimi nimshamba na hata nimevaa hizo nguo fupi bado wanasema hazina maadili hivyo mi nafanya ninachojisikia na waacha waendelee na malumbano yao,” aliongeza.