Limuru Starlets hao fainali Kombe la Wanyama

Muktasari:

Balozi wa michuano hiyo inayoshirikisha vijana wenye umri kati ya miaka 15-20, ni kiungo wa Tottenham Hotspurs na nahodha wa Harambee Stars, Victor Wanyama.

Nairobi. Timu ya Limuru Starlets kutoka Mjini Limuru imekuwa klabu ya kwanza kwa upande wa wanawake kutinga hatua ya fainali ya michuano ya kuibua vipaji nchini Kenya, maarufu kama Chapa Dimba.

Wanadada hao kutoka Limuru walijikatia tiketi baada ya kuwabandua Good Girls ya Thika kwa kuwatandika mabao 3-2 katika mchezo wa Nusu fainali ya kwanza  iliyopigwa kwenye uwanja wa Chuo cha ufundi cha Thika.

Good girls ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lakini kunako dakika ya kipindi cha kwanza kupitia kwa

Hata hivyo, Limuru Starlets waliamka na kusawazisha kupitia kwa Apondi Natalia (44).

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ile ile huku Limuru Starlets wakiendeleza mashambulizi katika lango la wapinzani wao na kujiandikia bao la pili kwa mkwaju wa penalti, likitiwa kimiani na Edwina Kwamboka (64), kabla ya kuongeza la tatu kupitia kwa kwa Muthoni Millicent (73).

Zikiwa zimesalia dakika tano mchezo umalizike, Good girls walicharuka na kuliandama lango la Limuru Starlets na kujiandikia bao la pili, mfungaji akiwa ni Wairimu Veronica (85).

Kwa ushindi huo Limuru Starlets imetangulia fainali na sasa inasubiri kukabiliana na mshindi wa Nusu fainali ya pili kati ya Rwambiti Girls na Express Queens

Mshindi wa fainali ya kesho atajikatia tiketi ya kushiriki fainali ya kitaifa itakayofanyika mwishoni mwa mwezi katika uwanja wa Bukhungu, katika kaunti ya Kakamega.

Balozi wa michuano hiyo inayoshirikisha vijana wenye umri kati ya miaka 15-20, ni kiungo wa Tottenham Hotspurs na nahodha wa Harambee Stars, Victor Wanyama.