Lilian ashinda taji la Miss Universe Tanzania 2017

Muktasari:

Mrembo huyo pamoja na kuongoza katika kura za mtandao bado ameshindwa kuingia katika 16 bora.

Dar es Salaam. Miss Universe Tanzania, Lilian Maraure  amelalamikia hatua ya majaji ya kutomuingiza hata katika hatua ya16 bora ya fainali hizo licha ya kuongoza katika kura za mitandao.

Lilian ambaye ni mtangazaji wa TBC international, alisema hayo mara alipowasili kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere kuwa miaka yote, warembo wanaongoza katika kura za mitandao upata nafasi ya kuingia katika hatua ya fainali tofauti na mwaka wake.

Alisema kuwa ameshangazwa hatua ya majaji ya kuwaingiza katika hatua ya 16 bora warembo ambao kuwenye kura za mitandao hawafanya vizuri na kumuacha wewe.

“Natambua kuwa uamuzi ya majaji ni ya mwisho, lakini nahoji hatua iliyochukuliwa ya kuacha kuingia hatua ya 16 bora na hata kwenye fainali pamoja na kupigiwa kura nyingi sana na kuongoza,” alisema Lilian.

Katika mashindano hayo, Mrembo wa Afrika Kusini, Demi-Leigh Nel-Peters alitwaa taji hilo.

Pamoja na matokeo hayo,Lilian alisema kuwa amepata uzoefu wa kutosha mbali ya kupata mikataba kadhaa ya kufanya maonyesho ya mavazi na ofa ya kusoma nchini Marekani.

Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communication, Maria Sarungi ambaye pia ni mratibu wa Taifa wa mashindano hayo, alisema kuwa wanayachukulia matokeo hayo kama changamoto na kuangalia zaidi mashindano yajayo.

“Ni kweli kuwa matokeo yanashangaza, hatujawahi kulalamika katika mashindano ya nyuma, safari hii tulihamasisha wadau watupigie kura nyingi, lakini matokeo ndiyo kama yalivyokuwa,” alisema Maria.

Maria alisema kuwa  wanasubiri kuambiwa lini mrembo ataenda Marekani kwa ajili ya kushiriki katika maonyesho ya mavazi na mkataba wa kusoma katika fani ambayo ataichagua.