Mchezaji Italia akojoa uwanjani

Muktasari:

  • Rais wa timu hiyo, Antonio Colantonio alikiri mchezaji wao kufanya kitendo kisicho cha kiuanamichezo na maadili lakini alilalamika adhabu kubwa iliyotolewa.

Mchezaji wa Ligi ya Seria D  kutoka klabu ya Turris Calcio nchini Italia, Giovanni Liberti amefungiwa mechi tano baada ya kukojoa kwenye eneo la mashabiki wa wapinzani wao.

Uongozi wa klabu hiyo umemtetea mchezaji huyo kwa kusema alibanwa na mkojo kutokana na kunywa maji mengi akiwa uwanjani.

Hata hivyo mchezaji huyo amefungiwa mechi tano kutokana na kitendo hicho kilichotokea wakati timu yake ilipokutana na Sarnese mechi iliyoisha kwa suluhu.