Lechantre ampa jezi yake Tshabalala

Monday April 16 2018

 

By Thobias Sebastian

Dar es Salaam. Kocha wa Simba, Pierre Lechantre leo atamwazisha nahodha msaidizi wa Simba, Mohammed Hussen 'Tshabalala' katika mchezo dhidi ya Prisons.

Tshabalala amekuwa na wakati mgumu katika kikosi cha Simba tangu alipotua beki Asante Kwasi aliyesajiliwa akitokea Lipuli katika dirisha dogo.

Lechantre alisema anafurahishwa na ushindani wanaonyesha Tshabalala na Kwasi wakiwa mazoezi kwani wote wanauwezo wa kama wanazidiana ni vitu vichache ambavyo kila binadamu anakuwa na kasoro yake.
"Kama kocha unapokuwa na wachezaji wawili ambao wapo katika kiwango cha juu na wanacheza sehemu moja ni nzuri sana katika timu ndio maana tangu nimekuja hapa namtumia Kwasi, lakini Tshabalala anakuwa katika wachezaji wa akiba," alisema.
"Nimempanga afanye mazoezi na kikosi cha kwanza kwani amecheza vizuri mechi na Mbeya City, lakini amekuwa akifanya vizuri katika mazoezi," alisema Lechantre.
Katika mazoezi ya mwisho ya Simba kikosi hiko kilionekana kucheza mfumo wao wa kawaida wa 3-5-2, ambao kipa Aishi Manula mabeki watatu watakuwa Yusuph Mlipili, Juuko Murshid na Erasto Nyoni, mabeki wa pembeni kulia ni Shomari Kapombe na kushoto Tshabalala.
Katika eneo la kiungo ni Jonas Mkude wakati mawinga wa kushoto na kulia ni Shiza Kichuya na Kwasi na washambuliaji ni Bocco na Okwi.