Larque: Pogba? Hatakiwi Ufaransa

Muktasari:

Larque alisema Pogba hastahili kabisa kupata nafasi katika timu ya taifa ya Ufaransa na hafahamu Kocha Didier Deschamps ametumia akili ya aina gani kumjumuisha staa huyo kwenye kikosi chake.

PARIS, UFARANSA

KIUNGO staa wa zamani wa Ufaransa, Jean-Michel Larque amesema supastaa wa Manchester United, Paul Pogba hakupaswa kabisa kuwa kwenye kikosi cha sasa cha Les Bleus.

Larque alisema Pogba hastahili kabisa kupata nafasi katika timu ya taifa ya Ufaransa na hafahamu Kocha Didier Deschamps ametumia akili ya aina gani kumjumuisha staa huyo kwenye kikosi chake.

Larque alisema: “Pogba? Ana bahati sana kuwa kwenye timu ya Ufaransa. Kwa kifupi tu, unapocheza ovyo kwenye klabu yako, huwezi kupata nafasi kwenye timu ya taifa.

“Pogba ana historia inayomruhusu kuwamo kwenye Timu ya Ufaransa. Tuwe wazi tu, timu ya Ufaransa si ya kujaribiana. Amekuwa kwenye timu kwa muda mrefu, lakini kwenye klabu yake hafanyi vizuri, hayupo vizuri.

“Sifahamu kwa nini kocha amelijumuisha jina lake kwa kuchagua mchezaji asiyekuwa na uwezo.

Pogba amepewa nafasi nyingi sana kwenye klabu yake, ameshindwa kuzitendea haki. Sasa amejumuishwa kwenye timu ya Ufaransa, lazima ajitathmini.”