Kwasi apima afya amevaa suruali ya Jeans, mkanda

Muktasari:

Wachezaji wa Simba wamefanyiwa vipimo vya afya leo kabla ya kuanza kwa safari yao ya kwenda katika ziara yao nchini Uturuki Jumapili hii.

Dar es Salaam. Beki wa Simba Mghana Asante Kwasi ametoa kali baada ya kufanyiwa vipimo vya afya akiwa amevaa suruali ya jean, mkanda na akiwa pekupeku.
Wachezaji wa Simba wamefanyiwa vipimo vya afya leo kabla ya kuanza kwa safari yao ya kwenda katika ziara yao nchini Uturuki Jumapili hii.
Upimaji wa afya za wachezaji hao ulifanyika katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam, lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida Kwasi akiwa amevalia jeans yake na mkanda alifanya vipimo hivyo.
Kwa kawaida wachezaji wanapofanyiwa vipimo vya afya huwa wanavaa nguo za kimichezo bukta au traksuti tofauti, lakini hali ilikuwa tofauti kwa wachezaji wa Simba ambao kila mtu alikuja amevaa kivyake.
Hivi karibuni Ronaldo alifanyiwa vipimo vya afya kabla ya kujiunga na Juventus alikuwa amevalia bukta na raba akiwa katika mashine ya kukimbilia.