Kuombwa fedha kwa mchosha Abedayor

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo amejikuta kwenye mgogoro mkubwa na familia yake kwa muda mrefu.

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Tottenham, Emmanuel Adebayor amesema alitaka kujiua tena kutokana na familia yake kumuomba fedha.

Nyota huyo wa zamani wa Manchester City alisema kila siku anapokea simu za kuombwa fedha bila ya kujali kuhusu afya yake.

Mshambuliaji huyo wa Togo (33) kwa sasa anacheza soka nchini Uturuki katika klabu ya Istanbul Basaksehir baada ya kucheza kwa muda Crystal Palace.

Alilimbia gazeti la Ufaransa ka So Foot: "Natamani kujiua kila wakati. Nimekuwa nikipambana na hali hii kwa miaka mingi peke yangu.

"Nachukia hali imefikia katika kiwango hiki, lakini najisikia nafuu ninapozungumza kuhusu suala hili.

"Muda wangu wa kucheza soka umebaki miaka mitatu au minne. Lakini jina langu la familia litabaki na mimi pamoja na watu hawa.

"Mambo yanakuwa magumu wakati unapojituma kuhakikisha familia yako inajiondoa katika umasikini, lakini bado watu hao hao wanakupiga.

"Kila siku namwambia mdogo wake tunafilisiwa na familia yetu.

"Mara kadhaa nimekuwa nalazimika kubadilisha namba yangu ya simu ili ndugu zangu wasinipigiea simu.

"Wanakupigia simu hawakuulizi hali yako, lakini wanataka uwape fedha. Hiyo ilijitokeza wakati nilipokuwa majeruhi Tottenham.