Kumbe tatizo lao Yanga linajulikana

Muktasari:

Abeid Mziba, straika wa zamani wa Yanga, anasema: “Kwanza kukosekana kwa Tambwe kunapunguza ushindani wa kuwania Kiatu cha Ufungaji Bora ambacho msimu uliopita kilichukuliwa na Simon Msuva na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting kwa kufunga idadi sawa ya mabao 14.”

KUKOSEKANA kwa straika wa kimataifa wa Yanga, Mrundi Amissi Tambwe ni tatizo kwenye fowadi ya timu hiyo iliyocheza mechi tatu, ikikusanyia mabao matatu kwa kushinda mechi moja dhidi ya Njombe Mji na kutoa sare mbili dhidi ya Lipuli na Majimaji.

Abeid Mziba, straika wa zamani wa Yanga, anasema: “Kwanza kukosekana kwa Tambwe kunapunguza ushindani wa kuwania Kiatu cha Ufungaji Bora ambacho msimu uliopita kilichukuliwa na Simon Msuva na Abdulrahman Mussa wa Ruvu Shooting kwa kufunga idadi sawa ya mabao 14.”

Lakini pia Mziba anasema licha ya Tambwe kutokuwa mpambanaji wa kuzunguka eneo kubwa la uwanja, ila ni hodari wa kutumia nafasi anazozipata kwa umakini.

Naye Ally Yusuph Tigana, alisema: “Sina maana kwamba wachezaji waliopo si wazuri, lakini kwa nafasi ya Tambwe kuna wakati unaona angekuwepo uwanjani kuna kitu angefanya na mambo yangekuwa tofauti.”