Klopp : Salah ana kazi kubwa!

Muktasari:

Salah amecheza soka la maana wakati kikosi chake kilipotoka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Roma katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana lakini Klopp anaona kwamba mchezaji huyo  bado ana kazi kubwa ya kufanya kufikia ubora wa dunia kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

LONDON, ENGLAND. JURGEN Klopp anaamini Mohamed Salah anatakiwa kucheza kwa kiwango cha juu kwa muda mrefu kabla ya kutazamwa kwamba ni mmoja kati ya wachezaji bora duniani.

Salah amecheza soka la maana wakati kikosi chake kilipotoka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Roma katika mechi ya kwanza ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya jana lakini Klopp anaona kwamba mchezaji huyo  bado ana kazi kubwa ya kufanya kufikia ubora wa dunia kama Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Kocha Klopp amesema: "Kuna wakati kila mtu husema lake, lakini kama unafahamu kwamba ni mchezaji bora au ana kiwango bora ni vizuri kuweka kila kitu hadharani."

“Ni kweli ana kiwango cha kimataifa, lakini mpaka uwe mchezaji bora wa dunia unatakiwa kuwa katika kasi na mafanikio kwa muda mrefu. Lakini kuna wachezaji wengine ambao wana kiwango kikubwa, ukichanganya na uwezo wake basi unapata mchanganyiko ulio bora,”anasema Klopp.