Kumbe Lechantre ana rekodi zake

KAMA kuna kitu utawakera mashabiki wa Simba ni kumsema vibaya kocha wao, Mfaransa Pierre Lechantre, ambaye amewafanya kutembea vifua mbele na kuwa na uhakika wa kubeba ndoo msimu huu.

Lechantre, ambaye amechukua mikoba ya Mcameroon, Joseph Omog ameiongoza Simba kwenye mechi sita za Ligi Kuu Bara bila kupoteza mchezo.

Mbali na kutopoteza mchezo, pia Simba imekuwa ikishinda kwa idadi kubwa ya mabao huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara chache na hilo, limewapa mzuka mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi. Iko hivi. Katika mechi hizo sita, Mfaransa huyo amevuna mabao 18 kwenye ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Majimaji, 3-0 kwa Ruvu, ikachomoza tena kwa 1-0 kwa Azam FC. Pia, walipata sare ya 2-2 na Mwadui FC, wakaipiga Mbao mabao 5-0 na kumaliza na sare iliyovuta hisia za mashabiki wa Yanga, ya mabao 3-3 dhidi ya Stand United. Hata hivyo, Simba imeruhusu wavu wake kuguswa mara tano, ambapo mfumo wake maarufu umekuwa ule wa 4-3-3. Wakati Simba ikiwa chini ya Omog, wavu wake ulitikiswa mara sita katika michezo sita, ambapo ni wastani wa bao moja kwa mchezo. Omog alipendelea zaidi kutumia mfumo wa 4-4-2. Katika uongozi wake, Omog aliiwezesha Simba kuvuna mabao 25 kwenye mechi 12 huku, michezo miwili iliyosimamiwa na kocha msaidizi, Mrundi Masoud Djuma, Simba ilivuna mabao sita kwa kuichapa Singida United mabao 4-0 kisha Kagera Sugar ikapigwa mabao 2-0.

Mfaransa Lechantre amechukua uongozi Simba ikiwa na mabao 31, ambapo akiongeza yake 18.