Kotei aivunja kambi ya makapera Simba kwa kufunga ndoa Ghana

Muktasari:

Kotei ambaye amecheza Simba kwa miezi sita, na kwa mafanikio makubwa ikiwemo kushinda taji la Kombe la FA, anaingia katika orodha ya wachezaji waliofunga pingu za maisha hivi karibuni.

 Hatimaye kiungo Mghana wa Simba, James Kotei amefunga pingu za maisha na mchumba wake wa muda mrefu Maltida Kwakye.

Kotei alianza kwa kufunga ndoa ya kimila siku ya Ijumaa na kisha Jumamosi kufunga ndoa kanisani.

Kotei ambaye amecheza Simba kwa miezi sita, na kwa mafanikio makubwa ikiwemo kushinda taji la Kombe la FA, anaingia katika orodha ya wachezaji waliofunga pingu za maisha hivi karibuni.

Wengine waliofunga pingu za maisha katika Ligi Kuu Bara ni Ibrahim Ajibu, Novatus Lufunga pamoja na Mohammed Samatta.