Kompany amvulia kofia Pep

Monday April 16 2018

 

London, England. Nahodha wa Manchester City, Vincent Kompany amedai ni fahari kubwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu England chini ya kocha Pep Guardiola.

Kompany aliwaongoza wachezaji wa timu hiyo kwenda kuponda raha ya kusherehekea ubingwa katika klabu ya Cheshire muda mfupi baada ya mahasimu wao Manchester United kufungwa bao 1-0 na West Bromwich Albion.

Baada ya kuiongoza Man City kutwaa ubingwa wa ligi mara tatu, nahodha huyo alisema ana matumaini Guardiola ataendelea kutwaa mataji mengine.

“Kwa mara ya kwanza kutwaa ubingwa, nadhani utaendelea kushinda mara nyingi. Unaposhindwa kwa mara ya kwanza unakata matumaini ya kushinda.

Libero huyo amesifu juhudi za wachezaji wenzake kucheza kwa kasi na kupata mafanikio msimu huu.

Pia, alidokeza amefurahishwa kutwaa ubingwa mbele ya mahasimu wao Manchester United baada ya kufungwa na West Brom.

“Lilikuwa bao zuri sana kutoka kwa Jay Rodriguez. Asante, alisema beki  huyo wa kati wa kimataifa wa Ubelgiji.

Awali, kabla ya matokeo hayo, Kompany alizungumza na Kyle Walker, Kevin De Bruyne kutafuta eneo la kusherehekea ubingwa.

Kocha Pep Guardiola aliwapa mapumziko ya siku tatu wachezaji wake  baada ya kupata ushindi dhidi ya Tottenham Hotspurs Jumamosi iliyopita.