Kombe la Rwakatare lafikia patamu Moro

Muktasari:

  • Klabu hiyo ni kati ya 80 zilizokuwa zikichuana ngazi ya awali ya mashindano hayo yanayohusisha timu za mkoa wa Morogoro.

Morogoro. TIMU 14 zimefuzu hatua ya 16 Bora ya michuano ya Kombe la Rwakatare Cup 2017 baada ya kufanya vizuri katika mechi zao za makundi ya vituo saba tofauti.

Klabu hiyo ni kati ya 80 zilizokuwa zikichuana ngazi ya awali ya mashindano hayo yanayohusisha timu za mkoa wa Morogoro.

Timu mbili za mwisho za kukamilisha idadi ya timu 16 zinatarajiwa kupatikana kupitia mechi za kituo cha Mang'ula.

Msimamizi Mkuu wa kituo cha Mngeta, Supertus Duma alisema timu 14 zimefuzu na kutinga hatua ya 16 bora baada ya kushika nafasi ya kwanza na pili katika makundi ya vituo hivyo saba vya Namawala, Mlimba, Mkamba, Ifakara, Mngeta na Chita.

Alisema wawakilishi wa Mang'ula watapatikana baada ya mechi zitakazopigwa Septemba 20 kabla ya timu hizo 16 kuanza kuonyeshana kazi kusaka bingwa wa michuano hiyo kwa mwaka huu.