Kombe la Dunia lasogezwa ‘live’ kiganjani

Muktasari:

Watumiaji wa mtandao wa Vodacom, watumiaji wataweza kupata maudhui yenye ubora wa kimataifa bila kukwama.

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kwa kushirikiana na Kwesé iflix, ambayo imeungana na Kampuni ya Econet Media ya utangazaji barani Afrika, wametangaza kuzinduliwa kwa mfumo wa kidijitali wa burudani utakaowezesha wateja wa Vodacom kuangalia mechi za Kombe la Dunia moja kwa moja katika simu zao za mkononi.
Watumiaji wa mtandao wa Vodacom, watumiaji wataweza kupata maudhui yenye ubora wa kimataifa bila kukwama.

Hii itawawezesha kushuhudia mechi za kombe la Dunia zinazoanza kesho Alhamisi jijini Moscow nchini Russia.
Huduma hii mpya ya Kwese iflix inawapa watumiaji burudani, ikijumuisha maudhui ambayo ni pamoja na utangazaji mubashara wa mashindano hayo makubwa ya kimataifa, ia vipindi vya kimataifa, kikanda na kitaifa ambazo zimelenga watazamaji wa Kiafrika.
Ikiwa na maelfu ya vipindi, maktaba kubwa ya Kwese iflix ina mengi, pamoja na vipindi vya kimataifa vinavyoonyeshwa kwa mara ya kwanza, vipindi vya televisheni vilivyoshinda tuzo mbali mbali na sinema maarufu kama vile ICE, Cleverman, Project Runway; Fashion Start Up S1, Confess pamoja na vipindi vinavyopendwa vya ndani kama vile Muoshwa huoshwa, Barua, Mama Huruma, Nabii Mswahili & Saa Mbovu na maudhui ya kikanda - Telenovela kama vile Goblin, Naagin and Bride of Habaek – vipindi vya watoto na maudhui mengine ya kimaisha. Huduma hii pia inawapatia waTanzania maudhui bora watakayoweza kuangalia bila gharama, ikiwa ni pamoja na tamthilia na vipindi vingine vya televisheni.
Wakitangaza kuzinduliwa kwa huduma hii, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kwese iflix, Mayur Patel, alisema, “Ikiwa ni ushirikiano baina ya watengeneza vipindi na watangazaji, Kwese na iflix, app ya Kwese iflix inawapa wateja burudani wakati wowote na mahali popote. Huduma hii imebuniwa kwa kizazi cha kidijitali, watumiaji sasa wanaweza kufikia vipindi vyao waviupendavyo vya michezo na televisheni bila kikomo na kwa njia inayoendana na maisha yao wakiwa katika mizunguko yao na kwa matakwa yao. Tunafura kushirikiana na Vodacom kufikisha maudhui yetu kwa Watanzania wengi zaidi.”
Akizungumzia ushirikiano huu, Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom, Nandi Mwiyombella alisema, “Huduma za video ndiyo zitaongoza siku zijazo katika mawasiliano na Kwese iflix itatuwezesha kutoa maudhui bora kabisa za kimataifa na kitaifa za michezo na burudani kwa wateja wetu.”

Mmoja wa waanzilishi wa iflix na Afisa Mtendaji Mkuu, Mark Britt aliongeza, “Tukio hili ni kubwa kwa iflix. Kwa pamoja na Econet Media, kampuni ya utangazaji inayoongoza barani Afrika, tumebuni huduma mahususi kwa ajili ya watumiaji wa kiAfrika, huduma ambayo itawawezesha watumiaji nchi nzima kujionea kila mechi ya Kombe la Dunia kupitia vifaa vyao. Huduma yetu ya Kwese iflix sasa ina maktaba kubwa kabisa ya maudhui ya burudani bora duniani, vyote vikipatikana kwa wakati mtumiaji anapotaka, tofauti na zamani.”