Kocha wa Nyanguge Combaini awazia ubingwa

Wednesday September 13 2017

 

By Saddam Sadick

Mwanza. Kocha wa Nyanguge Combine, Aureliani Stanslaus amesema kuwa akiifunga Alliance Queens basi anatangaza ubingwa kwani hakuna timu nyingine anayoihofia.
Ligi hiyo ambayo ilianza kutimua vumbi juzi Jumatatu kwenye Uwanja wa
Nyamagana jijini hapa, jumla ya timu tano zinapambana vikali kusaka
ubingwa wa Mkoa ili kushiriki ngazi ya kitaifa.
Aliongeza kuwa mapungufu yaliyopo kwa vijana wake atahakikisha anayafanyia kazi ili watakapoingia uwanjani wawe fiti kimapambano na
kwamba lengo lake ni kutwaa ubingwa.