Kocha Zahera ataka mechi ngumu zaidi

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema sasa hataki tena mechi laini badala yake ameagiza kutafutiwa mechi ngumu zaidi.

Zahera amesema sasa ni wakati wa kuona kikosi chake kikipimwa kwa kupata timu ngumu.

Zahera amesema anataka mechi hizo kuweza kujua ubora uliopo katika kikosi chake baada ya kukaa kambini kwa wiki moja na nusu.

Amesema  kwa sasa wachezaji wameimarika ambapo atahitaji mechi zisizopungua tatu ngumu.

Aidha kocha huyo raia wa DR Congo amesema angependa kupata mechi hizo kabla ya kukutana na USM Alger ya Algeria watakayokutana nayo jijini Dar es Salaam katika mechi ya hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.