Kocha Mourinho atetea kumwaga fedha usajili wa msimu huu

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho  amefunga na kusema kwamba suala la kutumia fedha nyingi wakati wa dirisha la usajili linakuwa nje ya uwezo wake licha ya kuwa tayari wametumia Pauni 106 milioni katika msimu huu wa kiangazi.

Mourinho amejitokeza kuzungumzia suala la fedha za usajili baada ya kumsajili Romelu Lukaku kwa gharama ya Pauni 75 milioni, huku Victor Lindelof akijiunga kwa kikosini hapo kwa Pauni 31 milioni.

Pia, klabu hiyo msimu ulioisha ilifanya usajili wa Pauni 89 milioni wa Paul Pogba ambao gharama hiyo iliongezeka hadi Pauni 109 baada ya kulipa na fedha ya wakala.