Kocha Mkongo wa Yanga ana mikwara huyo!

Muktasari:

Yanga ambayo imeweka kambi huko tangu wanzoni mwa wiki hii kujiandaa na mchezo huo ambao watacheza na mahasimu wao Simba.

KOCHA mpya wa Yanga, Zahera Mwinyi leo Jumatano ameanza rasmi kukinoa kikosi hicho katika mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Highland mkoani Morogoro basi unaambiwa ana mikwara kinoma.

Yanga ambayo imeweka kambi huko tangu wanzoni mwa wiki hii kujiandaa na mchezo huo ambao watacheza na mahasimu wao Simba.

Amefika uwanjani hapo na kuweka kikao cha dakika 8 akizungumza na benchi la ufundi na kuwaelekeza madhaa ambayo wao walikuwa makini kusikiliza.

Wakati wachezaji wakiwa wanapasha kwa kukimbia, kocha huyo alimwita Shadrack Nsajigwa na kuzungumza nae kwa takribani dakika 10 kisha akamwita tena na meneja wa Saleh Hafidh akazungumza naye.

 

AINA YA MAZOEZI

Mkongomani huyo aliongoza mazoezi ambayo yalikuwa ni kucheza mpira zaidi tena kwa spidi lakini anataka wakae na mpira kwa uhakika bila kupoteza kwa adui.

Zahera mara kwa mara amekuwa akimwita, Nsajigwa na kuelekezana nae huku Nsajigwa nae akimsikiliza kwa umakini.