Kocha Kerr awaita Simba mechi ya marudio na Yanga

Muktasari:

  • Kerr ambaye Jumatano ya wiki hii kikosi chake kiliichanachana Yanga ya Tanzania mabao 4-0,

CHUMA kimekolea moto, ndio tambo za kocha wa Gor Mahia, Dylan Kerr, aliyesema safari hii Afrika itawambua akiwatangazia hali ya hatari wapinzani wao Yanga katika Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Kerr ambaye Jumatano ya wiki hii kikosi chake kiliichanachana Yanga ya Tanzania mabao 4-0, kasema kuanzia sasa kila ajaye mbele yao awe amejiandaa kisaikolojia kabisa kwani hakuna atakayesalimika

Kocha huyo aliyewahi kufanya kazi Tanzania alipoifundisha Simba walio mahasimu wa Yanga, kawaalika mashabiki wa zamani wa huko Dar ili wajae uwanjani kushuhudia akiitia adabu tena Yanga.

“Ninajua itakuwa mechi ngumu kwa sababu Yanga watakuwa nyumbani na watahitaji kulinda heshima wakiwa pia na sapoti ya mashabiki wao, lakini presha itakuwa zaidi kwao na sisi tunajiimarisha zaidi,” alisema.

“Nawaalika Simba, naamini watakuwa upande wetu, nimezungumza na wawili watatu wakasema watakuja kwa fujo kutusapoti tuwatandike Yanga, nasi tutajitahidi kuhakikisha tunawapa raha hiyo.”