Kocha Harambee Stars ajipanga upya

Muktasari:

Kenya imefuzu kucheza fainali za Afcon mara tano, mara ya mwisho ilikuwa 2004

Nairobi. Kocha wa Harambee Stars, Paul Put anataka makocha wake wasaidizi, ukweli wa mambo umebainika.

Mbelgiji huyo amethibitisha kwenye mahojiano ya moja kwa moja na Mwanaspoti kuwa, amependekeza benchi lake la kiufundi ili kuboresha utendakazi wa Stars.

"Sijaanza kuwafuatilizia wachezaji wengi wa nje kwa sababu ligi zao hazijaanza, lakini kama Uhispania na England zinaendelea. Watu kama Olunga (Michael) wanafunzwa na makocha waliohitimu hivyo nasi ndio tuwafikie tunachokitaka lazima tuwe na benchi la nguvu

"Kufuzu michuano ya kimataifa si ajali, lazima uwe na watu wanaojua nini mnakifanya ndo sababu nikapendekeza waje makocha ambao, naweza kufanya nao kazi kwa urahisi. Si kusema kwamba, hawa niliokuwa nao hawajui lolote, la hasha bali tunataka kiwango cha juu,

"Ni wajibu wa FKF kupitisha pendekezo langu ili kazi iwe rahisi, " alifichua Put akiongeza Stars imepanga mechi nyingi za kirafiki na mataifa ya Congo, Mali, Nigeria au Burkina Faso kuanzia mwezi ujao.

Pia, atatumia mwezi Mei kujipima zaidi kwa ajili ya mechi ya Ghana mbio za kufuzu fainali za Mataifa Afrika (AFCON) mwakani.