Kocha AFC Leopard aanika siri ya ushindi kikosi chake

Monday September 11 2017

 

By Na THOMAS MATIKO

 KOCHA wa AFC Leopards, Robert Matano ‘The Lion’  , amesema matokeo mazuri  yanayoendelea kushuhudiwa tangu alipopewa majukumu hayo, yametokona  na sura ya kazi aliyowawekea wachezaji wake pale.

 Wikendi hii, mkufunzi huyo mwenye msimamo mkali uliompa lakabu ya The Lion, aliwaongoza vijana wake kuwalima Zoo Kericho 3-1, matokeo yanayofuatia sare ya 1-1  walipokabiliana na mashemejio Gor Mahia. Kabla ya kukabiliana na Gor, walikuwa wamewalima mabingwa watetezi wanaoteseka msimu huu Tusker 1-0.

 Kocha huyo kasema tatizo kubwa alilolikuta pale Ingwe ni utovu wa nidhamu kutoka kwa wachezaji na sasa kauondoa na ndio maana vijana wake wameonekana kuchangamka kweli kweli.

“Shida ya AFC ilikuwa utovu wa nidhamu na sasa nimeitoa na ndio maana mwaona matokeo tunayopata. Hakuna mchezaji yeyote mtovu wa nidhamu nitakayemchezesha na ninakuhakikishieni kwa kipindi,” alisema.