Kiungo wa Simba, aishukuru Mwadui

Muktasari:

"Kitendo cha Mwadui, kupewa nafasi ya kucheza ni bora zaidi kuliko nilipokuwa Simba, ilinitambulisha kwa watu, lakini maisha yangu yalikuwa ya benchi, wakati mwingine jukwaani,"

ALIYEKUWA kiungo wa Simba, Awadhi Juma amezungumzia mtazamo wake wa timu ya Mwadui FC, iliyomwajiri kwa sasa na kutamka kuwa imemfunza maisha halisi namna ambavyo anatakiwa kufanikiwa kisoka.

"Kitendo cha Mwadui, kupewa nafasi ya kucheza ni bora zaidi kuliko nilipokuwa Simba, ilinitambulisha kwa watu, lakini maisha yangu yalikuwa ya benchi, wakati mwingine jukwaani,"

"Bora uwezo wangu unijulishe kwa wadau wa soka, kuliko kujulikana na mashabiki wa Simba, wakati kiwango changu kingeendelea kudidimia siku hadi siku,kadri ninavyocheza ndivyo ninaweza kufika mbali zaidi ya hapa nilipo," anasema.

Awadhi anasema hawezi kujutia kuondoka Simba, bali anachukulia kama changamoto ya kujituma na kujua alikosea wapi hadi kupelekea kutohitaji huduma yake.

"Unajua katika maisha kila jambo ukachukulia kama shule, unakuwa na wakati mzuri wa kufanikiwa lakini kama utachukulia kwa chuki unakuwa unaua maono yako mwenyewe, kwani kocha hawezi kuacha mtu anayemsaidia,"anasema.