Lucho adaiwa kutaka kumua mkewe

Muktasari:

Nyota huyo wa Brazil ametamba akiwa na Porto na Marseille wakati akicheza soka Ulaya

Curitiba, Brazil. Polisi imethibisha kuwanza kumchunguza kiungo wa zamani wa Porto na Marseille, Lucho Gonzalez kwa madai ya kutaka kuumua mkewe.

Tukio hilo lilitokea Desemba 8, polisi wakiwa umbali wa mita 500 kutoka nyumbani kwa Gonzalez waliwahi eneo hilo na kumzuia kuwaona watoto kwa siku 90 kutokana na suala hilo.

"Mume wangu, Lucho González, alijaribu kutaka kuniua," Andreia da Silva Marques Gonzalez aliimbia Globoesporte.

"Tulikuwa tukibishana ndipo alipojaribu kutaka kuniua. Tulikuwa tunazungumza huku akiwa ananisukuma mara kadhaa, kabla ya kunitupa kitandani na kunikaba shingo yangu kwa mikono miwili na kupiga kilele: Nitakuua nitakuua!'

"Aliwahita watoto wetu wawili chumbani na kuwaambia: 'Njooni muone mama yenu kichaa anavyokufa."

“Baada ya hapo aliichukua kila kitu nyumbani pamoja na dhahabu zangu, fedha kutoka akaunti zangu, na kuzifunga kadi zangu za benki.