Kiungo Simba kufanyiwa mabadiliko

Muktasari:

  • Aussems ambaye katika mechi zake za kirafiki na Ligi Kuu Bara amekuwa akiwatumia viungo kama, Hassan Dilunga, Mghana  James Kotei na Jonas Mkude zaidi na wengine kama Said Ndemla na Mdhamiru Yassin wakikosa kabisa nafasi.

Mtwara. Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amepanga kuifanyia mabadiliko safu yake ya kiungo na kuwatumia wenye uwezo wa kuwachezesha washambuliaji.

Aussems ambaye katika mechi zake za kirafiki na Ligi Kuu Bara amekuwa akiwatumia viungo kama, Hassan Dilunga, Mghana  James Kotei na Jonas Mkude zaidi na wengine kama Said Ndemla na Mdhamiru Yassin wakikosa kabisa nafasi.

Mbali na hao, Simba ina viungo wengine kama Mzambia Cletus Chama ambaye alikosa nafasi ya kucheza kwa sababu ya kibali cha kazi kuchelewa kufika kutoka Zambia na Mohamed Ibrahim 'Mo' ambaye ameanza kupewa nafasi sasa.

"Nitaongeza nguvu katika eneo la kiungo ushambuliaji ili kutengeneza nafasi za kufunga nyingi zaidi, mbali na mipira ya krosi ambazo tumekuwa tukizitumia," alisema Aussems ambaye ni Mbelgiji.

Amesema, yatakuwa mabadiliko madogo tu ambayo kama kocha ameyaona.

Simba ilianza vizuri katika mechi zao za awali kwa kuzifunga timu za Tanzania Prisons na Mbeya City kabla ya kumaliza suluhu na Ndanda jana Jumamosi.