Kisa Uwanja: Tottenham yaomba radhi mashabiki

Muktasari:

  • Katika taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa muda mfupi uliopita, ilisema imesikitika sana kushindwa kuufungua uwanja huo wa Tottenham Hotspur Stadium kama ilivyoahidi awali.

London, England. Klabu ya Tottenham Hotspur, imewaomba radhi mashabiki wake kwa kuchelewa kufungua uwanja wao baada ya kuufanyia ukarabati.

Katika taarifa ya klabu hiyo iliyotolewa muda mfupi uliopita, ilisema imesikitika sana kushindwa kuufungua uwanja huo wa Tottenham Hotspur Stadium kama ilivyoahidi awali.

Taarifa hiyo ilisema kuwa uwanja huo sasa utafunguliwa baadaye na sio Septemba mwaka huu, kama walivyoahidi awali lakini utapokamilika utakuwa na viwango vya kutumika kwa mechi za Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

“Tottenham inawaomba radhi masabiki wake kwa kuchelewa kuufungua uwanja wake, tunasikitika sana lakini ni ukweli kuwa ilishindikana kwa sababu zilizo nje ya uwezo wetu,” ilisema taarifa hiyo.

Katika taarifa hiyo Spurs imesema inasikitika kushindwa kuufungua uwanja huo Septemba 15 kwa mchezo wa Ligi Kuu watakaoikaribisha Liverpool, ambao sasa kama ilivyoopangwa ambapo sasa utafanyika kwenye uwanja wa Wembley.

Ili kuepuka kuwachanganya mashabiki timu hiyo imeamua kuuhamisha hata mchezo kati yake na Cardiff City utakaofanyika Oktoba 6 mwaka huu ambao nao sasa utafanyika kwenye dimba la Wembley.