Agyei kipa bora Ethiopia

Muktasari:

Agyei ambaye aliidakia Simba kwa mafanikio lakini ikatokea sintofahamu Wekundu wa Msimbazi wakaachana naye na kuwasajili makipa wengine ambao ni  Aishi Manula, Said Mohemed 'Nduda' na Emmanuel Mseja.

Mlinda mlango wa zamani wa Simba, Mghana Daniel Agyei amechaguliwa kuwa kipa bora wa Ligi Kuu ya Ethiopia msimu huu.
Agyei ambaye aliidakia Simba kwa mafanikio lakini ikatokea sintofahamu Wekundu wa Msimbazi wakaachana naye na kuwasajili makipa wengine ambao ni  Aishi Manula, Said Mohemed 'Nduda' na Emmanuel Mseja.
Lakini, Agyei alipoona Simba wamemkatia mawasiliano, akapata 'dili' nchini Ethiopia katika klabu ya Jimma Ketema FC ambako tangu kipindi hicho amecheza kwa kujituma na kumaliza akiwa kinara.
Agyei alisajiliwa Simba pamoja na Mghana mwenzake James Kotei ambaye bado yuko katika kikosi hicho kilichotangaza
ubingwa msimu huu.