Kipa Indonesia afia uwanjani

Muktasari:

  • Kipa huyo aligongana na mwenzake na kupasuka kichwani na shingoni

Jakarta, Indonesia. Kipa wa timu ya Persela Lamongan, Choirul Huda amefariki baada ya yakugongana na mchezaji wa Semen Padang, Ramon Rodrigues wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Indonesia uliochezwa Jumapili.

Kipa huyo alikutwa na mauti hayo muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini.

Awali mchezaji huyo alipata jeraha kubwa kichwani na shingoni vitu ambavyo vilionekana wazi kutishia maisha yake.

Awali daktari aliyemuhudumia, Yudistiro Andri Nugroho alisema ajali hiyo ilisababisha mchezaji huyo apate maumivu makali kifuani na shingoni na wakati huo huo mapigo ya moyo yakasimama.

Hata hivyo wakati kipa huyo akikimbizwa hospitalini mechi iliiendelea na Persela ikaishinda Semen Padang kwa mabao 2-0.

Huda 38, alikuwa mkongwe wa klabu hiyo akicheza jumla ya mechi 500 tangu alipojiunga kwa mara ya kwanza mwaka 1999.