Kimweri kumdeku Dula Mbabe Taifa

Muktasari:

  • Kimweri pia amepanga kugawa vifaa vya michezo kwa mabondia watakaopigana kwenye pambano hilo litakalochezwa Uwanja wa Ndani wa Taifa chini ya waandaaji Super D Boxing chini ya Rajab Mhamila ‘Super D’.

BONDIA Mtanzania anayefanya shughuli zake nchini Australia, Omari Kimweri ametua nchini na anatarajiwa kushuhudia pambano la kukata na shoka kati ya Fred Sayuni na Haidari Mchanjo litakalofanyika Jumapili ijayo jijini Dar es Salaam.

Kimweri pia amepanga kugawa vifaa vya michezo kwa mabondia watakaopigana kwenye pambano hilo litakalochezwa Uwanja wa Ndani wa Taifa chini ya waandaaji Super D Boxing chini ya Rajab Mhamila ‘Super D’.

Mratibu wa mapambano hayo, Super D alisema Kimweri ametua nchini juzi kwa ajili ya pambano hili akiwa na vifaa vya kupigania siku hiyo kama sehemu ya mchango wake katika mchezo huo na kukumbuka alipotokea kabla ya kuwa bondia wa kimataifa.

Mbali na pambano la Sayuni na Mchanjo, siku hiyo pia kutakuwa na burudani ya aina yake wakati Abdallah Pazi ‘Dula Mbabe’ ataonyeshana kazi na George Dimoso, huku Vincent Mbilinyi na Said Kidedea watamalizana kimtindo katika pigano jingine.

Mapambano mengine ni lile la Mohamedi Kashinde dhidi ya Sadiki Momba, Issa Nampepeche atatavaana na Faraji Sayuni na Bakar Mbede atapimana mbavu na Frank John, huku Super D akiwahimiza mashabiki kujitokeza kwa wingi siku hiyo.