Kili Stars kamili Kenya

KIKOSI cha Kilimanjaro Stars chini ya Kocha Mkuu,  Ammy Ninje,  kinaondoka mchana huu wa saa 07:15,  kwenda Nairobi, Kenya, tayari kwa michuano ya Kombe la Chalenji, inayotarajiwa kuanza wikiendi hii.

Wachezaji na benchi la ufundi la kikosi hicho, wanaondoka nchini wakiwa na matarajio makubwa ya kufanya vizuri na watafungua michuano hiyo Jumapili dhidi ya  Libya.

"Tunakwenda Kenya na lengo moja la kuhakikisha tufanya vizuri katika michuano hiyo na kuiletea sifa nchi yetu,"alisema Ninje.

Kilimanjaro Stars imepangwa Kundi ‘A’ pamoja wenyeji Kenya, Rwanda na timu alikwa ya Libya kutoka Kaskazini mwa Afrika, imeshatwaa taji hilo la Chalenji mara tatu tangu ilipoanzishwa.

Kikosi kilichoondoka wachezaji ni makipa Ramadhani Kabwili (Yanga), Aishi Manula (Simba SC) na Peter Manyika (Singida United).

Mabeki ni Gadiel Michael (Young Africans), Boniphace Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Young Africans), Kennedy Juma (Singida United), Erasto Nyoni (Simba SC), Mohammed Hussein (Simba SC) na Amani Kiata  (Nakuru All Stars ya Kenya).

Viungo wa kati ni Himid Mao ambaye ni Nahodha (Azam FC), Jonas Mkude (Simba SC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin (Simba SC), Raphael Daud (Young Africans), Shizza Kichuya (Simba SC), Abdul Hilal (Tusker/Kenya) na Ibrahim Ajib (Young Africans).

Washambuliaji ni Mbaraka Yussuph na Yahya Zayed (Azam FC), Elias Maguri (Dhofar/Mascat, Oman), Daniel Lyanga (Fanja FC/Mascat) na Yohana Mkomola (Ngorongoro Heroes).

Benchi la Ufundi linaundwa na yeye Ninje ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja), Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).