Vumbi la ubingwa wa mkoa lashika kasi

Muktasari:

  • Mashindano hayo yanalengo la kupata timu moja itakayowakilisha mkoa huo katika mashindano ya taifa

Timu ya Eagles Queens imeitembezea kichapo cha pointi 21-20 J.Mond kwenye mashindano ya mpira wa Kikapu yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Kiloleli jijini Mwanza.

Mchezo huo uliopigwa majira ya saa nne asubuhi, ulikuwa mkali kwa timu zote kuonyesha umwamba, lakini Eagle.

Michezo mingine Young Eagle iliichapa Young Profile kwa pointi  22-13, Bwiru Boys ikailaza Pasiansi Sekondari pointi 28-12 na Young Profile ikaitandika Kiloleli pointi 28-12.

 Nayo Young Spider ilikubali kichapo wa pointi 21-19 dhidi ya Bwiru Boys,Young J.Mond ikailaza Young Eagle Queens pointi 16-6 na Kiloleli Sekondari ikaichapa Young Spider pointi 26-17.

 Mratibu wa mashindano hayo Mkoa wa Mwanza, Bahati Kizito alisema kuwa lengo la mashindano hayo ni kupata timu moja itakayowakilisha Mkoa kwenye michuano ya kitaifa yatakayofanyika Desemba mwaka huu jijini Dar es Salaam.

 Alisema Mikoa itakayoshiriki ni sita ambayo ina programu ya kuendeleza mchezo wa Kikapu ikiwa ni Dar es Salaam, Iringa, Kigoma, Dodoma, Arusha na Mwanza.

 “Awali tulizindua programu ya kuendeleza mchezo wa kikapu kwa timu za hapa mkoani, tumewaleta vijana wote waonyeshe uwezo wao ili tupate timu moja itakayowakilisha Mkoa,”alisema Kizito.

Aliwaomba wadau nchini kujitokeza kwa wingi kusapoti mchezo huo kama ilivyo katika soka kwa manufaa ya vijana na Taifa kwa ujumla.