Kigogo aitosa Arsenal atua AC Milan

Muktasari:

  • Kuondoka kwa Gazidis kumethibitishwa na Arsenal ambayo tayari imeshaziba nafasi yake

London, England. Mkurugenzi Mtendaji wa Arsenal, Ivan Gazidis ameachana na klabu hiyo na kutimkia AC Milan.

Gazidis aliyeitumikia Arsenal kwa miaka tisa, kabla ya hapo alikuwa ni Kaimu Kamishna Mkuu wa Ligi Kuu ya soka nchini Marekani (MLS).

Taarifa za kuondoka kwa Gazidis zimethibitishwa na Arsenal ambayo tayari imeshaziba nafasi yake huku pia ikifanya mabadiliko madogo katika usimamizi wa klabu.

Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Biashara ya Arsenal, Vinai Venkatesham ameteuliwa kuziba nafasi ya Ukurugenzi Utendaji iliyoachwa na Gazidis.

Aliyekuwa Mkuu wa Idara ya mahusiano ya soka, Raul Sanllehi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Utawala wa mpira wa miguu ndani ya klabu hiyo.