Kigogo Yanga yamkuta TFF, Kidau freshi

Muktasari:

"Yanga walileta barua ya kukataa kwa mwenyekiti wao si Sanga bali ni Yusuph Manji kwahiyo hana sifa kuu ya kuwa katika nafasi hiyo," alisema Karia.

Dar es Salaam. Kamati tendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), chini ya mwenyekiti wake Rais Wallace Karia imekubaliana kumsimamisha Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, Clement Sanga kwa kukosa sifa ya stahili.

"Yanga walileta barua ya kukataa kwa mwenyekiti wao si Sanga bali ni Yusuph Manji kwahiyo hana sifa kuu ya kuwa katika nafasi hiyo," alisema Karia.

"Tutaanza michakato wa kutafuta mwenyekiti mpya ili kuziba nafasi hiyo ambayo kwa sasa ipo wazi kwa kufanya uchaguzi kama ilivyokuwa hapo awali, " alisema Karia.

Baada ya hilo Karia alisema kikao cha kamati Tendaji imelizia na kukubaliana kwamba Wilfred Kidau aliyekuwa anakaimu nafasi ya Katibu Mkuu amethibitishwa rasmi.

Karia alisema wataboresha ratiba ya Kombe la FA kutoka timu 80, hadi kufikia mia na zaidi, timu za Ligi Kuu kuwa na timu za vijana chini ya umri wa miaka 17-20 ambapo kutakuwa na ligi yao inayoendelea.

Anasema wataboresha Ligi daraja la kwanza ambapo kutakuwa na timu 24 ambazo zitakuwa katika makundi mawili na zile za kwanza katika kila kundi zitapanda Ligi Kuu moja kwa moja pia na Ligi daraja la pili wanafika kuboresha.