Kiduku anaondoka Mtibwa Sugar

Muktasari:

  • Kiduku maarufu kwa ufungaji wa mabao ya adhabu kama penalti na faulo.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Kelvin Sabato 'Kiduku' ameomba kuondoka ndani ya kikosi hicho cha wakata miwa wa Manungu, Morogoro ili akajiunge na timu nyingine.

Kiduku maarufu kwa ufungaji wa mabao ya adhabu kama penalti na faulo.

Ameomba kuondoka ndani ya kikosi hicho kwa lengo la kwenda kutafuta timu nje ya nchi.

Kiduku amesema: "Ni kweli nimeomba kuondoka na lengo langu ni kwenda kutafuta timu ya kucheza nje ya nchi."

Amesema, kama mambo yake yataenda vizuri ataondoka kwenda kwenye majaribio na ikishindikana atarudi.