Kichuya ataondoka kwa maelewano

Saturday August 12 2017

 

By Fredrick Nwaka,

Dar es Salaam. Afisa Habari wa Simba,  Haji Manara alisema klabu hiyo haijaafikiana na mawakala wa mchezaji Shiza Kichuya ili kumpeleka kucheza soka la kulipwa nchini Misri.

"Wakija na ofa tunayotaka wala hatuna shida, Simba tuna utamaduni wa kuuza wachezaji,"alisema Haji bila kutaja kiasi ambacho Simba inahitaji.

MCL Digital lilizungumza na Kichuya ambapo alisema yeye ni mchezaji na ataufanyia kazi uamuzi utakaoafikiwa baina ya klabu yake na mawakala na kusisitiza anafurahia maisha kweny kikosi cha Simba.

Klabu ya Etihad ya Misri ndiyo inayotajwa kuwania saini ya Kichuya baada ya kumuona kwenye mashindano ya Cosafa yaliyofanyika nchini Afrika Kusini mwezi uliopita.

Pia,  Manara alisisitiza kuwa beki Juuko Murshid bado mchezaji wa Simba na atakiwa kuripoti Dar es Salaam kabla timu haijaenda Zanzibar.

"Bado ana mkataba na sisi wenzetu walitaka afanye majaribio, lakini sisi tuliona muda unakwenda na tunamhitaji kikosini,"alifafanua Haji.