Kiba na mkewe kula fungate hapa

MAMBO tayari mwanangu! Ndio, King Kiba tayari amebeba jiko pale Mitaa ya Kongowea mjini Mombasa, leo alfajiri lakini amekupa na saprize ya maana tu.

Baada ya kufunga ndoa hiyo akiwa amesindikizwa na swahiba wake Gavana wa Mombasa, Hassan Joho na mdogo wake, Abdu Kiba, unajua fungate ya Kiba na mkewe Amina Khaleef itakuwa wapi?

Iko hivi. Baadaye sherehe ya nguvu itakayofanyika Aprili 29 jijini Dar es Salaam, Kiba atabeba mkewe na kuelekea nchini Italia kwa ajili ya fungate. Unajua atakwenda kutulia hoteli gani? Endelea kutembelea mtandao wa Mwanaspoti kwa habari zaidi.