Kha! Mshahara wa Sterling balaa

Muktasari:

Kwa nyongeza hiyo anayotaka Sterling kwenye mshahara wake ina maana atakuwa akilipwa Pauni 275,000 kwa wiki, kwa sababu kwa sasa kiasi anachovuna kila wiki ni Pauni 175,000

MANCHESTER, ENGLAND.RAHEEM Sterling anapima maji kwa ujiti huko Manchester City. Waweza kusema hivyo baada ya winga huyo kuripotiwa kwamba anataka nyongeza ya Pauni 100,000 kwenye mshahara wake wa wiki ili asaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake Etihad.
Kwa nyongeza hiyo anayotaka Sterling kwenye mshahara wake ina maana atakuwa akilipwa Pauni 275,000 kwa wiki, kwa sababu kwa sasa kiasi anachovuna kila wiki ni Pauni 175,000.
Taarifa zilizopatikana ni kwamba Sterling yupo tayari kubaki kwenye kikosi hicho, lakini anachotaka ni kwamba na yeye alipwe mshahara kama wa Kevin De Bruyne, ambaye ndiye analipwa mshahara wa kibosi kwenye timu hiyo ya Etihad.
Man City wamekuwa na wasiwasi na ile sheria ya matumizi ya pesa ya Uefa, lakini wamekuwa na kawaida ya kutoa marupurupu mengine kwenye mshahara ikiwamo haki za taswira, bonasi na ada ya usajili ambayo inawekwa kwenye mkataba kumfanya mchezaji kuvuna pesa ndefu kwa wiki. Kama Sterling atakubali kusaini dili jipya basi ataungana na wachezaji ambao watakuwa kwenye timu hiyo kwa muda mrefu kama David Silva, Fernandinho, Gabriel Jesus na kipa Ederson.