Kenya mabingwa wapya London 7s

Nairobi. Hatimaye yametimia. Hii ndio kauli unayoweza itumia unapozungumzia matokeo waliyoyapata timu ya taifa ya Kenya ya Raga, kwa wachezaji saba kila upande, Shujaa 7s.
Habari njema ni kwamba, baada ya kuondolewa kwenye taji kuu, Kenya imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Challenge huku ikijizolea alama 101 na hivyo kuweka rekodi mpya ya kufikisha alama 100, kwa mara ya kwanza katika historia ya huo nchini.
Awali kabla ya kuelekea England, kocha wa Shujaa 7s, Innocent Simiyu aliahidi kuwa kikosi chake kitaweka historia kwenye mrururu huo, ahadi ambayo imetimia jana usiku baada ya kukusanya alama nane katika ushindi wa 39-19, dhidi ya Wales kwenye mchezo mkali wa fainali.
Ushindi wa Kenya ulipatikana kupitia kwa Jeff Oluoch aliyepiga trai mbili, huku Eden Agero, Willy Ambaka na Collins Injera nao wakifanya yao na kuipa Kenya ubingwa huo muhimu, kuelekea jijini Paris, kwa ajili ya msururu wa mwisho wa msimu huu wa mchezo wa Raga, Paris 7s.
Safari ya Kenya kuelekea fainali ya Kombe la Challenge ilianza na ushind wa 42-10 dhidi ya Argentina, katika hatua ya nusu fainali, ambapo waliandikisha alama 100. Katika hatua ya robo fainali, iliyopigwa mapema leo asubuhi, Kenya iliitandika Hispania 37-0.
Hata hivyo, licha ya kuweka historia hiyo, Kenya imejikuta ikishuka katika msimamo wa ubora duniani kutoka nafasi ya sita hadi nafasi saba. Wenyeji England wamepanda hadi nafasi sita na alama zao 103, huku nafasi ya tano ikienda kwa marekani (alama 105).
Katika nafasi ya kwenye msimamo ni New Zealand. Mabingwa wa taji kuu, Fiji wanaendelea kutanua katika nafasi ya kwanza baada ya kufikisha alama 160, alama saba juu ya Afrika Kusini inayoshika nafasi ya pili kwa ubora duniani wakiwa na alama 153.
Wakati huo huo, makundi ya Paris 7s imetoka ambapo Kenya imepangwa katika kundi la kifo linalojumuisha Timu ya Fiji ambao ni mabingwa wa London 7s, pamoja na New Zealand na Samoa. Wote wako kundi A.
Makundi ya Paris 7s
Kundi A: Fiji, New Zealand, Kenya, Samoa.
Kundi B: Afrika Kusini, Canada, Russia, Scotland.
Kundi C: Ireland, Australia, Wales, Hispania.
Kundi D: England, Marekani, Argentina, Ufaransa.