Nditi na Mtibwa wana siri nzito

Muktasari:

Katwila ambaye alicheza kikosi kimoja na Nditi kabla ya kupewa ubosi huo amesema, Nditi mwenye miaka 34 ambaye pia ni nahodha wa timu, katika nafasi ya kiungo anayocheza,  amekuwa kiunganishi mzuri kati ya safu  ya ulinzi na ushambuliaji na ndiyo maana wanafanikiwa.

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zubeiry Katwila amesema, sababu ya kutomweka benchi kiungo wake, Shaaban Nditi tangu msimu wa ligi kuu ulipoanza, ni msaada alionao ndani ya timu.
Katwila ambaye alicheza kikosi kimoja na Nditi kabla ya kupewa ubosi huo amesema, Nditi mwenye miaka 34 ambaye pia ni nahodha wa timu, katika nafasi ya kiungo anayocheza,  amekuwa kiunganishi mzuri kati ya safu  ya ulinzi na ushambuliaji na ndiyo maana wanafanikiwa.
 "Nditi anapata nafasi katika timu ni kutokana na kujitoa kwake lakini pia ni kiongozi kwa wenzake kwa kila kitu.Huwezi kumtumia mchezaji mmoja katika mechi zote lazima atakuwa na kitu cha ziada,”alisema Katwila.
“Nditi, pia kama unavyojua,  yeye ni mchezaji mzoefu na anautumia uzoefu wake vizuri na kuwa mfano kwa wachezaji vijana."
Nditi alijiunga na Mtibwa Sugar  mwaka 2002, msimu wa 2006 alisajiliwa na Simba na miaka miwili baadaye, aliachana nao akarudi Mtibwa anayoichezea mpaka sasa.