Mtibwa: Tunapambana na hali yetu

Muktasari:

Mtibwa ambayo ilifungwa na Kagera Sugar bao 1-0, nyumbani kwao Manungu, timu ambayo inafundishwa, Mecky Maxime,  kocha aliyewahi kuichezea na kuifundisha  klabu hiyo maarufu kama Wanatamtam miaka ya nyuma.

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zubeiry Katwila amesema, kikosi chao hakijajiondoa kwenye mbio za kuwania ubingwa, kilichotokea ni hali ya mchezo na sasa wanapambana na hali yao kuhakikisha wanarudi kileleni.
Mtibwa ambayo ilifungwa na Kagera Sugar bao 1-0, nyumbani kwao Manungu, timu ambayo inafundishwa, Mecky Maxime,  kocha aliyewahi kuichezea na kuifundisha  klabu hiyo maarufu kama Wanatamtam miaka ya nyuma.
Alisema: "Hatujakata tamaa, sisi tunapambana na hali yetu bwana, lengo ni kuhakikisha tunarudi kwenye mstari kama tulivyofanya mechi za awali. Kufungwa ndiyo maana ya ligi, leo unapoteza, kesho unashinda, unatoa sare ni kawaida lakini si kwamba ndiyo tumejitoa."
Kwa sasa Mtibwa inashika nafasi ya nne na pointi 17,  nyuma Simba inayoongoza ligi na pointi  22 sawa na za  Azam FC inayoshika nafasi ya pili wakati Yanga inashika nafasi ya tatu na pointi 20.