Kaseke ajiamini kucheza chini ya kocha Pluijm

Muktasari:

  • Alifafanua kauli yake kwamba alitumia umakini kufanya uamuzi wa kutathmini timu ya kuichezea msimu ujao na kuamua kusaini maiaka miwili Singida badala ya Yanga na Mwadui.

Winga wa zamani wa Yanga, Deus Kaseke ametaja sababu iliyomfanya atue Singida United iliyo chini ya kocha Hans Pluijm kwamba ni usajili wao.

Alifafanua kauli yake kwamba alitumia umakini kufanya uamuzi wa kutathmini timu ya kuichezea msimu ujao na kuamua kusaini maiaka miwili Singida badala ya Yanga na Mwadui.

"Ni kweli kwamba wachezaji wengi wanaangalia dau, lakini hilo haliwezi kumfanya mchezaji awe bora, Singida wamesajili kikosi chenye ushindani ambao utanifanya nijituma kwa bidii," alisema

Kaseke alisema katika timu yake mpya yupo kocha Pluijm ambaye anajua kuwajenga wachezaji kuamini bidii kwamba ndiyo inayozaa mafanikio, hivyo anaamini kwamba hajapotea njia.

"Uwezo wa Pluijm, unajulikana kwa namna ambavyo ameisaidia Yanga, kitu pekee anapenda timu kuwa na umoja, mchezaji kujituma bila kujali timu inapitia mawimbi gani kwamba uwezo ndiyo unaweza kumnufaisha,"alisema.