VIDEO-Karia: Sina urafiki na fedha za TFF

Muktasari:

  • Kamati ya Maadili imemsimamisha maisha Makamu Rais wa Shirikisho la Soka (TFF) Michael Wambura kwa makosa matatu ya kimaadili.

 Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema mtu yeyote atakayecheze na fedha za shirikisho hilo hatamuacha hata kama ni rafiki yake.

Karia ametoa kauli hiyo wakati kukiwa na mjadala mkali kuhusu kufungiwa maisha kwa makamu wake wa Rais wa Michael Wambura akidaiwa kupokea na kuchukua fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo  hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013.”

Akizungumza jijini leo Karia alisema kamati ya maadili inaweza  kufanya majukumu yake kwa  kunihoji kama kutakuwa na shitaka linalonihusu, Blatter (Sepp) alihukumiwa na kamati yake.

"Uongozi wetu ulikuwa na sintofahamu, Fifa ilituma watu na kufanya ukaguzi kwa sababu tulikuwa bado hatujaaminika..., tuhakikishe tunashirikiana ili tupate fedha za kuendelea soka na ujenzi wa kituo chetu.., hatuna usiri, kila tunachofanya tuna weka wazi.

"Mimi ni binadamu kama nikikosea naweza kuadhibiwa kama Blatter na kama nitafanya vyongo naweza kujiengua kwenye nafasi hii, " Karia.

Rekodi ya Ammy Ninje hii hapa ameitaja Karia.

"Anazaidi ya wachezaji 10 ambao wamepita kwenye mikono yake wanacheza Ligi Kuu Uingereza, Ninje amekuwa akifundisha timu za vijana kule, analeseni ya Uefa. "

"Nisipangiwe wa kufanya naye kazi, ujinga na fedha sitaki, nikikosea niambiwe, " alimaliza Karia kwa kusisitiza.