Liverpool yamvaa Kane wa Spurs

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo wa England amekuwa na msimu nzuri akisaidia Spurs katika msimamo wa Ligi Kuu

Liverpool, England.KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp ameingilia mjadala wa nani mkali kati ya washambuliaji Harry Kane na Romelu Lukaku akisema Kane kiboko yao.

Klopp alitoa kauli hiyo wakati alipojiandaa kumkabili Kane na kikosi chake cha Tottenham Hotspur leo Jumapili katika mchezo wa Ligi Kuu England uliotarajiwa kufanyika uwanjani Wembley.

Liverpool ilimdhibiti vizuri Lukaku wa Manchester United katika mchezo uliomalizika kwa suluhu kwenye Uwanja Anfield wikiendi iliyopita.

“Sitaki kuwa jaji wa wawili hawa. Wote ni mastraika mahiri,” alisema.

“Tofauti kali yao ni kwamba Harry anakuwa kwenye sehemu ya mchezo zaidi hata kama atakuwa hajafunga –lakini nadhani hata Lukaku anaweza kufanya hivyo pia.

“Tulimnyima mipira Lukaku, lakini kufanya hivyo kwa Harry kutatoa nafasi kwa Dele Alli na Eriksen ambao wapo kila mahali uwanjani na wanapiga mashuti kutoka umbali wowote. Pamoja na yote hayo, Harry si mshambuliaji bora tu Ulaya bali duniani.”

Kwa rekodi za msimu huu kabla ya mechi za jana, Kane amefunga mabao sita na hana asisti, wakati Lukaku amefunga mabao saba na asisti mbili.